Red +Meat = Kansa? Habari za kuhofisha kwa wanaopenda nyama.

Red Meat
Red Meat
  Wataalam  wa kansa wana habari mbaya zaidi kwa wanaopenda nyama nyekundu  na vyakula vilivyotengezwa kwa ngano –ambavyo  wengi wanaamini ni vyakula vya uzunguni . Wataalam wanasema  utafiti umethibitisha kwamba   aina hio mbili ya vyakula huzidisha sana uwezekano wa  kansa ya koloni au colorectal  kwa wanawake na wanaume .

Nyama nyekundu  ni baadhi ya vyakula vyenye utata sana katika historia ya lishe  lakini  Dr Nazik Hammad  amewaambia wanahabari kwamba Nyama haijalengwa kwa hila  ." Kansa ya koloni ua Colorectal cancer  haukuwa ugonjwa wa kawaida barani afrika  lakini  sasa umekithiri kwa sababu watu wameacha vyakula vya kienyeji kama vile nafaka ,mboga na matunda ili kutegemea lishe ya kisasa ya vyakula vya uzunguni  ambavyo ni rahisi kutayarisha’ amesema   Dkt  Nazik .

 Tafiti zaidi zinazidi kuthibitisha kwamba kuna uhusiano mkubwa  kati ya lishe inayotumiwa na watu na aina ya magonjwa ya kisasa kama vile kansa ,kisukari na   shinikizo la damu . Sukari , Vyakula vyenye chumvi nyingi na vyenye kemikali ni baadhi ya sababu zilizotajwa kwa ongezeko la visa vya ugonjwa wa kansa . Pia wanaofanya mazoezi wana fursa nzuri ya kupunguza uwezekano wa kupatwa na kansa .

 Hayo yakiarifiwa Taasisi ya kitaifa ya Saratani imechapisha ripoti inayoeleza viwango vya maradhi ya saratani katika kila kaunti, hatua ambayo taasisi hiyo inasema itachochea serikali kubuni sera mwafaka kukabili ugonjwa huo. Ripoti hiyo ambayo imewasilishwa kwa kamati ya bunge ya Afya na afisa mkuu mtendaji wa taasisi hiyo Alfred Kiragu imeweka peupe aina za saratani zinazo waathiri wanaume na wanawake katika baadhi ya kaunti nchini.

Kulingana na ripoti hiyo saratani ya koo na ile ya korodani zinaongoza katika maambukizi ya satarani miongoni mwa wanaume katika kaunti 11 zilizoorodheshwa. Kaunti hizo ni: Nairobi, Kisumu, Meru, Mombasa, Kakamega, Kiambu, Nyeri, Nakuru, Bomet, Embu na Eldoret.

Saratani ya koo au ya umio ndio inayoongoza nchini na kuna visa vingi vya saratani hiyo katika kaunti za Kisumu, Kakamega, Nyeri, Nakuru, Bomet na Eldoret, ikiathiri wanaume na wanawake kulingana na taasisi ya kensa nchini.Saratani ya matiti inaongoza miongoni mwa wanawake katika kaunti hizo teule 11.Kulingana na ripoti hiyo, maambukizi ya kensa ya matiti ni mengi mno katika kaunti za Nairobi, Meru, Mombasa, Kiambu, Nakuru na Embu. Katika kaunti ya Nairobi wanaume wengi waonakabiliwa na hatari ya kuugua saratani ya korodani kwa asilimia 32.1 ikifuatwa na ile ya umio kwa asilimia 12.8.