dianibeach

RED ZONE: Uingereza yawatahadharisha raia wake kuja Kenya .

Serikali ya Uingereza imewaonya raia wake dhidi ya kuja nchini Kenya kwa sababu ‘magaidi wanaweza kutekeleza mashambulizi’.Raia  wa Uingereza wanaokuja Kenya  wametakiwa kuwa waangalifu  wakizuru maeneo ambayo watalii  huyapenda kama vile hoteli ,mikahawa ,maduka ya jumla ,vilabu vya usiku  na majengo ya kibiashara yenye shughuli nyingi. Maeneo ya kuabudu kama vile  makanisa na miskiti pia yanaweza kulengwa . Ilani hiyo  imezitaja kaunti  za kaskazini mashariki kama vile Garissa na mandera na baadhi ya  maeneo ya  Tana River na Lamu  kama sehemu ambazo  raia wa Uingereza hawafai kwenda iwapo ziara hizo sio muhimu .

CRIMINAL or VICTIM? Ufichuzi watolewa kuhusu mwalimu aliyeuawa na mwili wake kuchomwa Kitui .

Ilani hiyo ya usafiri ambayo ilitolewa jumamosi haijazihusisha ziara za watali mbugani  na maeno ya fuo za bahari pwani . Visiwa vya lamu na Manda pia vimeachw anje ya tahadhari hiyo . Kulingana na  afisini ya  FCO ambayo hutoa ilani hizo ,takriban  wakaazi 190,000 wa Uingereza huzuru Kenya bila kupata matatizo yoyote. Ilani hiyo inajiri wiki moja baada ya magaidi kushambulia kambi ya kijeshi  ya manda-magogoni inayotumiwa na wanajeshi wa Kenya na Marekani  huko Lamu . Shambulizi hilo lilitishia kuvuruga mojawapo ya vitega uchumi muhimu sana kwa Kenya –Utalii kwa sababu ya wageni wengi wa kutoka mataifa ya nje ambao huzuru pwani ya Kenya .

Photo Credits: The Star

Read More:

Comments

comments