Redio Jambo yatua miji ya Nyeri na Mwea kuzawadi mashabiki

Sonko wa masonko amewashangaza wakaazi wa miji ya Nyeri na Mwea kwa baraka za hela mifukoni hii leo. Katika zoezi na ambalo linatazamiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu wa Agosti, kituo kinachoongoza nchini kwa matangazo ya kuaminika kimepanga misururu ya ziara lengo kuu ikiwa ni kuwatunuku mashabiki hela.

Cha muhimu sonko huyu hutaka kujua ni iwapo wasikilizaji wanaelewa kabisa maneno machache yanayolipa senti "The Phrase That Pays". Iwapo shabiki ataweza kung'amua Redio Jambo Ongea Usikike,sonko huwatuza shilingi 1,000. Aidha, mashabiki wanaozidisha ubunifu na kuyaandika maneno hayo katika bango hutunukiwa shilingi 5,000 pesa taslimu.

Sonko anatarajiwa kuzuru maeneo ya kaunti ya Kirinyaga hususan Kerugoya hapo kesho na baadaye kuzamia mji wa Embu masaa ya alasiri.

Tazama picha za baadhi ya washindi na mashabiki wa miji ya Nyeri na Mwea: