‘Release my brother!’Nduguye Omar Lali aomba kuachiliwa kwake baada ya mazishi ya Tecra

Siku chache baada ya mwanawe mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Keroche Breweries Tecra Muigai kuzikwa ,mpenzi wake Omar Lali angali anazuiliwa.

Omar alikamatwa kwa baada ya kuhusishwa na  kifo cha Tecra .

Kulingana na upasuaji wa mwili wa mwendazake ,iliripotiwa kuwa   alianguka kutoka kwa gazi la nyumba yao,na kupata majeraha yaliyosababisha kifo chake.

Tecra aliaga alipokuwa anaendelea kupokea matibabu, huku majeraha yaliyokuwa kwenye upande wake wa kushoto yakisababisha kifo cha mwendazake.

Sasa nduguye mdogo wa Omar  Quswai Lali Omar, anataka ndugu yake achiliwe huru, kupitia mitandao ya kijamii ya twitter Quswai aliandika.

"RELEASE MY BROTHER OMAR!! A GOOD CARING DAD AND OUR MENTOR!! HE HAS BEEN ALWAYS GOOD TO US INCLUDING THE LATE TECRA MUIGAI. MAY ALMIGHTY PROTECT YOU AND COME BACK HOME SAFE!!” Aliandika.

Quswai alisema kuwa ni mtoto wa kumi na moja katika familia ya Lali, anafanya kazi katika hoteli ya Peponi kaunti ya Lamu na amesomea useremala.

Mbali na hilo rafiki yake Mohamed Bin Shaib aliandika haya;

“ALTHOUGH YOU ARE BEHIND THE BARS, WE STILL WISH YOU A HAPPY EID MUBARACK! BE STRONG AND KEEP SMILING!!! THE PRESIDENT OF LOVE!!”