‘Remember to go home early’, mashabiki wamwambia Betty Kyallo

Mwanahabari wa runinga ya K24 Betty Kyallo anaendelea na maisha yake na kujifurahisha awezavyo licha ya kukosolewa na mashabiki wake katika mitandao ya kijamii.

Mwanahabari huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja anasemwa sana katika mitandao ya kijamii nchini kwa kila hatua anayopiga maishani na kile anachokifanya kila siku.

Hata mtoto wa darasa la sita anamfahamu kwa sana.

Kila Betty anapokosolewa na mashabiki wake ama kukejeliwa huwa anawajibu awezavyo bila ya kufikiria majibu yake mitandaoni.

Betty aliweka picha yake katika mtandao akiwa amevalia mavazi ya kimahajabu ilhali hakufafanua alipokuwa, lakini mashabiki wake hawakukimya bali walimkejeli.

Wengi wao walipendezwa na urembo wake bali si wote mmoja aliandika;

"Remeber to go home early after all." Joel Aliandika.

Hakufua dafu alimjibu na kumuuliza yeye ni nani wa kumkumbusha aende nyumbani.

"@Jo.el3953 and whi are you to lecture me😅." Betty alimjibu.

Betty amekuwa akijibu kejeli yeyote ambayo inamuhusu na inahusu maisha yake.

Akiongea awali katika mahojiano Betty alikuwa na haya ya kusema,

"Niliacha kujali na kukasirikia wanao nichukia kwa sababu kila mtu anang'ang'ana na jambo moja au lingine katika maisha yao, hamna mtu ambaye ni kamili hii maisha

Ata mimi si kamili, wengi uwa wanasema Betty nataka kuwa na furaha kama wewe, lakini hawajui changamoto na kung'ang'ana nimepitia ili niwe na furaha

Hata matajiri wa matajiri ana ng'ang'ana na jambo fulani, kwa hivyo niliamua kupuuza kejeli za watu, ninapoona jambo ambalo linaweza kunisaidia uwa nalichukua vyema katika maisha yangu

Lakini jambo ambalo halinisaidii uwa nakufa moyo na siamini katika kuchukia watu." Betty Alizungumza.