32322916_195883451043494_6176234134961127424_n-696x464

Rich Mavoko : Sioni mtu wa kuomba msamaha WCB

Staa wa muziki wa Bongo fleva Rich mavoko amedokeza kuwa haoni wa kumwomba msamaha katika lebo ya WCB. Mavoko alitoka ghafla katika lebo hiyo inayoongozwa na nyota na mwanamuziki mkubwa Afrika Diamond Platnumz.

Wasanii wengine walio chini ya usimamizi wa lebo hiyo ni pamoja na Harmonize, Rayvanyy, QueenDarleen na mkali Mbosso.

Soma hadithi nyingine:

HopeKid : Nilifukuzwa kanisani kisa skendo yangu na DK kwenye Beat

download

Mgogoro na mvutano mkubwa ulifuata kuhusu mtakaba aliokuwa ameingia na usimamizi wa lebo hii ya Wasafi. Kulingana na Mavoko, mkataba wake na WCB ulivurugika kipindi baadhi ya vitu alivyotaka havikufanywa na lebo hiyo.

Soma upate uhondo hapa:

Hopekid reveals student in threesome scandal with DK Kwenye Beat was suicidal

” Mkataba bado haujaisha ata kama nimetoka. Kuna baadhi ya vitu havikwenda sawa na nilivyotaka mimi. Nilikaa sana na nyimbo na ambazo nilitakiwa nizitoe ila sikuweza. Kuna kipindi mamangu alinipigia kuniulizia mbona sitoi nyimbo. Sikuona kabisa maisha mazuri ya usoni nikiwa WCB.” alisema Mavoko.

Staa huyu anayetamba na nyimbo mpya inayofanya vizuri Usiguze amesema kuwa hawezi kurudi lebo aliyotoka katika mahojiano na kituo kimoja nchini Tanzania. Kuhusu kuomba msamaha na kukubali kurudi katika lebo hiyo kubwa Afrika mashariki, staa huyu alisema hawezi kabisa.

“Nilipoingia WCB sikuona msanii mkubwa hapo ukiweka kando mkubwa wa lebo hiyo. Naomba msamaha wa nini? Kosa gani nilifanya mimi? Sina matatizo na yeyote WCB.”

 

lucy2

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments