Rihanna ndiye mwana muziki tajiri wa kike Duniani

Rihanna
Rihanna
Rihanna  ameibuka kama mwanamuziki tajiri sana wa kike duniani  huku thamani ya mali yake ikikisiwa kupaa kuwaliko  vikongwe katika muziki wa pop - Madonna, Céline Dion  na  Beyoncé.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31  ambaye jina lake halisi ni  Robyn Rihanna Fenty,  ana mali yenye thamani ya  Dola milioni 600 kulingana na Forbes –na kumpiku  Madonna  kwa dola milioni 30  ,Dion kwa pauni milioni 150 na Beyonce kwa dola milioni 200 .

Rihanna ambaye anafahamika sana kwa nyimbo zake tajika kama vile  "Umbrella," "Diamonds" na  "What's My Name?,"  hajapata mali yake kupitia muziki pekee .

Kulingana  na Forbes  pesa zake nyingi zimetokana na ushirikiano wake na kampuni ya Ufaransa ya  LVMH ambayo hutengeza bidhaa za  mvuto na   vipodozi  zenye  majina mazito kama vile Christian Dior, Givenchy na  Louis Vuitton.

Mwezi uliopita ,staa huyo wa  Barbados  alizindua leb yake ya fashoni  Fenty  katika mji wa  Paris  na kuwa mwanamke wa kwanza meusi  kuunda nembo halisi kwa ushirikiano na   LVMH.

Fenty  ndio biashara ya hivi punde ya Rihanna  baada ya kuzindua  nyingine kama vile  Savage X Fenty,  mwaka jana  na  Fenty Beauty ya kuunda vipodozi  mwaka wa 2017

Biashara hiyo ya nguo ndio yake ya kwanza katika  soko la mavazi ya kifahari  ingawaje amekuwa akiwatengezea nguo za kisasa wateja wa Uingereza kama vile  River Island  na alitangazwa kuwa mkurugenzi wa Ubunifu  wa Puma mwaka wa 2014 .

Miradi mingine ya  biashara za Rihanna imesifiwa  kwa  uwezo wa kuwashirikusha watu mbali mbali na matabaki tofauti .  kampuni yake ya vipodozi  ,imeunda aina 40 ya rangi  ilahli ile inayotengeza nguo za ndani  ina aina nyingi zinazoambatana na maoumbo tofauti ya watu . kampuni yake ya fashoni inamudu hata wanawake wenye  kiwango cha size 14 (Marekani)