Msaani wa Gospel Ringtone amemtumia mwenzake Bahati ujumbe mkali kupitia facebook akimshtumu kwa kuwa na kiburi na dharua . Ringtone kupitia ujumbe huo anasema Bahati hajakuwa kielelezo kizuri kwa jamii na hasa kwa wasanii wa muziki wa injili nchini kutoka na majibizano yake makali na wenzake pamoja na wafuasi wake katika mitandao ya kijamii .
Bahati alimpeleka kortini Msanii Peter Blessing baada ya wawili hao kutofautiana na hivi maajuzi amerushiana matusi na msanii G money .