RIP: Mauaji ya wakili Chesang kutokana na chachu za mipango ya biashara

1896690(2)
1896690(2)
Ni mauaji ambayo yalikuwa yamewaacha wengi na maswali yasiyo na majibu, polisi ambao wanachunguza mauaji ya ukatili ya wakili Robert Chesang wanaamini yalikuwa ya mipango ya biashara ambayo haikuenda ilivyotakikana.

Chesang, 45, alipigwa risasi nyumbani wake Moke Gardens Lukenya, kaunti ya Machakos, wauaji hao waliweza kuwateka nyara walinzi wa mali hiyo.

Kisha kuwaambiwa waweze kuwaonyesha nyumbani kwa wakili huyo. Mmoja wao alipokataa madai yao aliweza kupigwa na nyuma ya bunduki ya AK47 katika jicho lake.

Polisi walisema kuwa wakili Robert alikuwa amehusika na manunuzi ya ardhi, hii ni moja wapo wanasema inaweza kuwa ilisababisha kifo chake.

Mkubwa wa DCIO wa kaunti ya Machakos George Kisaka na mkubwa wa polisi wa Athi-river Sharma Wario walisema kuwa wawili hao inaonekana walikuwa wamjetumwa ama kuajiriwa kumuua.

"Mauaji hayo yalifanyika kati ya saa 11:30 asubuhi na 12:30 adhuhuri, walimteka mlinzi ili kuwaelekeza nyumbani kwa Chesang," Alisema Wario.

"Walipowasili katika maeneo ya Chesang mmoja wao alibisha mlango wakili huyo aliweza kuangalia kwa dirisha, kisha mmoja wa wauaji hao alimpiga risasi tatu mfululizo katika kifua," Aliongeza Wario.

Wakili huyo aliishi peke yake na mke wake ambaye ni hakimu katika kaunti ya Nyeri kuishi na watoto wao wawili katika maeneo hayo ya Nyeri.

Polisi waliweza kupata mwili wa marehemu sebuleni ukiwa na damu kila mahali na nyaraka kutawanyika katika kiti chake, kompyuta ya mkononi, vitabu na vijitabu vikiwa vimetapakaa kila mahali.

Inaweza kuwa walikuwa wanatafuta nyaraka muhimu, na kuzipata kisha kutoroka nazo ama ilikuwa mauaji ya sababu nyingine?

"Inamaana kuwa ni watu ambao waliteuliwa ambao wanaojua kutumia bunduki za AK47, pengine shirika hali, inaonekana wakili alikuwa anaishi kwa uoga kwa maana badala ya kufungu mlango alichungulia kwa dirisha," Alisema Sharma.

Washambulizi hao waliweza kutoroka bila kubeba kitu chochote na kuwaacha walinzi hao wakiwa wamewafunga na kamba katika maeneo hayo.

Wario alisema kuwa hawajajua kiini cha mauaji hayo, na hajaweza kutawala kuwa mauaji hayo yametokana na mipango ya biashara.

Hakuna mshukiwa yeyote ambaye ameweza kukamatwa kufikia jana, iliwekwa wazi kuwa mwaka jana Chesang aliweza kushtakiwa katika mahakama ya Mavoko kwa kumuumiza mke wake.

Mke wake Maisy Omungala aliweza kuuliza mahakama iweze kumlinda kutoka kwa mume wake ambaye alikuwa vurugu.