Sanz

RIP: Rais wa zamani wa Real Madrid afariki baada ya kuambukizwa coronavirus

Aliyekuwa rais wa kilabu ya soka ya Real Madrid Lorenzo Sanz  aliaga dunia siku ya jumamosi baada ya kulazwa hospitalini akiugua virusi vya Corona .

Sanz mwenye umri wa miaka 76  alikuwa rais wa kilabu hiyo ya  Bernabeu  kutoka 1995-2000,  kipindi ambacho Real Madrid ilishinda kombe la mabingwa mara mbili .

” Babangu ameaga dunia ‘ aliandika mwanawe Sanz Lorenzo Sanz  Duran katika Twitter .

” hakustahili kufika mwisho katika hali hii . mmoja wapo ya watu wajasiri na wenye bidii ambaye nimewahi kuwaona katika maisha yangu .Familia yake na kilabu ya Real Madrid ni vitu alivyovipenda sana’

Sanz aliwasajili wachezaji kama vile Roberto Carlos , Clarence Seedorf na  Davor Suker wakati wa hatamu yake .

 

 

 

 

Photo Credits: Radio Jambo

Read More:

Comments

comments