Ripoti ya Sarah Cohen, Maelezo ya unyama aliyotendewa na Tob

unnamed__1___1569830017_59586
unnamed__1___1569830017_59586
Taarifa zipo kwamba Tob Cohen alisusa mpango wa kumpa mkewe Sarah shilingi 50,000 kila mwisho wa mwezi kuanzia Januari mwaka huu.

Hii ni kwa mujibu wa stakabadhi za korti.

Stakabadhi za Sarah zinaonyesha kuwa Cohen ndiye alianzisha juhudi za kutafuta talaka.

Sarah anadai kuwa wao wawili walianzisha kampuni ya TOBS Limited mwaka wa 1991.

Soma hadithi nyingine:

Cohen alikuwa mwenyekiti, Sarah alikuwa mkurugenzi mkuu.

Kufuatia matatizo ya ndoa yao, Tob aliacha kumlipa mshahara wake kuanzia Januari.

Mjane Sarah anaonyesha picha ya ndoa iliyojaa mateso huku mmewe akimfanyia unyama atoke kwenye nyumba.

Sarah anasema kuwa Cohen alizidi kumnyima mshahara wake akifahamu kuwa hana pahali pengine pa kutoa riziki.

Soma hadithi nyingine:

Cohen,71, alifika kortini akitaka talaka baada ya kuibua tetesi kuwa mkewe alikuwa anampiga na kumnyima tendo la ndoa.

Cohen alisema kuwa ndoa hiyo haingeweza kuendelea kitu na ambacho Sarah amekubali katika stakabadhi zake za majibu.

Wairimu ni mshukiwa wa mauaji ya mmewe na anatakiwa kufika mahakamani Jumanne.

Sarah analalamika kuwa Cohen alikuwa anamtusi kwa misingi ya rangi ya ngozi.

Soma hadithi nyingine:

Wairimu anasema kuwa alikuwa anahisi upweke mwingi pale chumbani.

Bwanake Cohen angemuacha peke yake wikendi na kuenda kucheza mchezo wa gofu na wanawake wengine.

Zaidi ya hapo, Sarah anasema kuwa mmewe alimtenga na familia yake kwa sababu hangeweza hakuelewa lugha ya Kikuyu.

Sarah anaongeza kuwa mmewe angetoka kulewa usiku mzima halafu anaingia nyumbani alfajiri na kumtupia matusi ya kila aina.