crime_scene_tape

RIP: Polisi kuchunguza mauaji ya wakili Robert Chesang

Milio ya risasi ilisikika, si risasi tu pekee zilikuwa zinapigwa hewani kama kawaida ni mwanadamu alikuwa anauwawa na majinai wasiojulikana kwanini walikuwa wanampiga risasi wakili Robert Chesang.

Polisi wanachunguza kisa hicho cha mauaji ya wakili huyo aliyepigwa risasi hadi kifo nyumbani kwake Lukenya kaunti ya Machakos.

1490413(2)

Patanisho: Wewe unakaa mkia wa umbwa unafuata huku huku Bi Carol alipuka

Robert Chesang alipigwa risasi Jumapili na wanaume wenye walikuwa na bunduki ya aina ya AK47  mchana nyumbani kwake Moke Gardens na kisha watu hao kutoroka.

Polisi walisema kuwa walipojulishwa kuhusu tukio hilo waliweza kuenda eneo hilo kisha kupata lango kuu na milango ya Robert Chesang imefunga.

Inasemekana kuwa Chesang alikuwa peke yake tukio hilo ilipokuwa inafanyika, polisi waliweza kupata cha kiasi cha risasi saba ambazo zilitumika kutoka katika bunduki ya AK47.

 

Dandora activist Caroline Mwatha’s father speaks out over abortion autopsy

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuifadhi maiti cha Shallom, Athiriver katika kaunti ya Machakos.

Kwanini wauwaji hao wamuuwe wakili huyo na walijua aje alikokuwa anaishi ina maana kuwa walikuwa wametumwa ama walikuwa wanataka ninin kutoka kwa wakili Robert Chesang?

Ni maswali ambayo familia na marafiki pia wananchi wanajiuliza kwa sasa.

Manchester United players mobbed by fans as they take the train

Jamii ya sheria ya Kenya (law Society of Kenya) waliweza kuonya kwa maneno makali zaidi kitendo cha mauaji hayo.

“Tunamuita inspeckta mkuu wa polisi na vifaa vya usalama vya nchi waweze kwa haraka kuanzisha uchunguzi wa mauaji hayo ya Robert Chesang na kisha kupena matukio kwa haraka, na kuhakikisha haki imetendeka,” Alisema LSK.

Jamii ya sheria ya Kenya waliweza kuomboleza na familia hiyo ya mwendazake wakili Robert Chesang, ilihakikishia familia ya wakili huyo kusimama na kuwasaidia katika wakati huu mgumu ambao wanaopitia kwa kumpoteza mmoja wao.

 

Photo Credits: the star

Read More:

Comments

comments