Waititu alizaliwa januari tarehe 1 mwaka wa 1962 na safari yake katika siasa ilianza mwaka wa 2002 alipchaguliwa diwani wa Njiru kupitia chama cha KANU . Katika uchaguzi mkuu wa 2007 aliamua kuwania ubunge Embakasi dhidi ya kigogo David Mwenje na mwanasiasa aliyekuwa mgeni kwa siasa za eneo hilo Meritus Mugabe . Katika uchaguzi huo Mugabe Were aliwashinda Waititu na Mwenje lakini kwa bahati mabay akauawa katika tukio la wizi nje ya lango lake mtaani Woodley hata kabla ya kuapishwa januari tarehe 29 mwaka wa 2009 .
Katika uchaguzi mdogo ulioafuatia Waititu alinyakua ushindi na kateuliwa kuwa wazri msaidizi katika serikali ya muungano .Baadaye alipokonywa wadhfa huo baada ya kukabiliwa na madai ya uchochezi . Mwaka wa 2013 Babayo aliamua kuwania kiti cha ugavana jijini Nairobi kupitia tiketi ya TNA lakini akashindwa na Evans Kidero wa ODM .Wenzake katika kundi la TNA Mike Sonko na Rachael Shebesh waliushinda viti vya Seneta na mwakilishi wa akina mama mtawalia . Mapema mwaka wa 2015 aliwashangaza wengi alipotangaza kwamba sasa atahamia Kiambu ili kuwania kiti cha eneo bunge la Kabete baada ya kuuawa kwa mbunge wa eneo hilo George Muchai . Alishinda kiti hicho katika uchaguzi mdogo na akapata ujasiri sasa wa kupiga hatua nyingine .Alitangaza kwamba atawania ugavana ili kumbandua Gavana wa kwanza wa Kiambu William Kabogo .Kabogo alimpuuza kama mtu asiyeweza kumpa ushindan wala kumtoa kijasho lakini Babayao alipombwaga katika uchaguzi wa mchujo kuwania tiketi ya chama cha Jubilee , tayari guu lake moja lilikuwa katika afisi ya gavana .
Hakupata pumzi Waititu kwani pindi tu baada ya kuapishwa kama gavana ,tofauti ikaibuka kati yake na naibu wake James Nyoro na washirika wake kadhaa waliomsaidia kukishinda kiti hicho .Patashika ya hapa na pale na mgogoro wa uongozi pamoja na vita vya ndani kwa ndani hatimaye vilimzidi maarifa Babayao.Masaibu yake yaliwekwa mafuta yamtelezeshe vizri wakati waakilishi wa kaunti ya Kiambu walipopitisha hoja ya kumfurusha kwa tuhuma za kujinufaisha kutumia kandarasi ,utumizi mbaya wa fedha za umma na kutumia vibaya maamlaka ya afisi yake .Babayao alipewa fursa kufika senate ili kujitetea dhidi ya madai hayo.Aliwaraia maseneta kumsaza na hata akaawambia siku moja watakuwa magavana na yeye atakuwa seneta kwa hivyo wamhurumie lakini ng’o! Kauli ikawa kumwondolea jina la gavana na kumrejesha katika meza ya kujipanga upya . Hayajaishia hapo-Waititu yungali ana kesi ya kujibu kortini kuhusu madai yaliyotolewa na waakilishi wa kaunti ya Kiambu .