Robert Mugabe azikwe Heroes Acre au Zvimba, suluhu ya mzozo yatolewa

Hatimaye familia ya rais wa kwanza wa Zimbabwe, Robert Mugabe imefikia hali ya kuelewana na serikali kuhusu atakapozikwa.

Pande hizi mbili zimezika tofauti baada ya majadiliano ya muda.

Serikali ilikuwa na msimamo ya kuuzika mwili huo katika makaburi yaliyozikwa mashujaa wakombozi wa taifa hilo.

Soma hadithi nyingine:

Mugabe alifariki katika hospitali moja nchini Singapore alipokuwa akipata matibabu kwa muda mrefu.

Afya yake Robert ilianza kunyong’onyea kwa kipindi kirefu.

Wanahabari nchini humo waliwahi kufurushwa wakitaka kumhoji katika hali ya ugonjwa.

Haya yanajiri baada ya ibada ya mazishi kufanyika katika mji mkuu wa Harare.

Serikali ilikuwa imepinga ombi la shujaa huyu kuzikwa nyumbani kwake.

Soma hadithi nyingine:

 Hadi kwa sasa haijaweza kubainika ni kwa nini Robert Mugabe hafai kuzikwa katika makaburi ya Heroes Acre.

Mipango ilikuwepo ya kujenga mnara wa makumbusho wa kumuenzi kiongozi huyo wa kwanza wa Zimbabwe.

Serikali sasa inashikilia kuwa itaheshimu uamuzi wa familia ya marehemu.

Waziri wa Mawasiliano Nick Mangwana alichapisha kauli katika mtandao wa Twitter kuonyesha msimamo wa serikali.

Mvutano wa familia na serikali huenda unachochewa na dhana kuwa kiongozi huyo aling'olewa madarakani na mshirika wake, wa zamani Rais Mnangagwa, miaka miwili iliyopita.