Ronaldo afunga mabao 4 huku Ureno wakiwanyuka Lithuania 1-5

ronaldo
ronaldo
Cristiano Ronaldo alifunga mabao manne Ureno walipowanyuka Lithuania 5-1 katika mechi ya kufuzu kwa Uro mwaka 2020.

Kiungo huyo wa Juventus sasa amefunga mabao 93 ya kimataifa, 16 nyuma ya rekodi ya dunia ya raia wa Iran gwiji Ali Daei. Matokeo haya yanaiweka Ureno katika nafasi ya kufuzu moja kwa moja, wakiwa alama tano nyuma ya viongozi wa kundi B Ukraine.

Serbia wamepanda hadi katika nafasi ya tatu kwenye kundi hilo baada ya kuwanyuka Luxemborg 3-1.

Kwingineko, Henrikh Mkhitaryan anasema ilimlazimu kuondoka Arsenal ili kupata furaha ya kucheza soka tena, alipojiunga na Roma kwa mkopo msimu huu wa joto.

Alijiunga na Gunners kutoka Manchester United mwaka wa 2018, na kufunga mabao 8 tu kati ya mechi 39 za ligi. Raia huyo wa Armenia, ambaye alifungia nchi yake mabao mawili walipochuana na Bosnia jumapili, anahisi ni kama alikua lazima kwake kuondoka Uingereza ili kupata tena upendo wake kwa soka.

Matumaini ya Somalia ya kushinda awamu ya makundi ya kufuzu kwa kombe la dunia kwa mara ya kwanza yalifikia kikomo baada ya kunyukwa na Zimbabwe jijini Harare.

Ocean Stars walikua na nafasi nzuri baada ya kushinda mechi ya awali 1-0 na kushinda mechi hio kwa mara ya kwanza katika michuano hio. Zimbabwe walianza kufunga baada ya dakika 77 kabla ya Somalia kusawazisha kupitia kwa Omar Abdullahi.

Tukirejea nchini, nahodha wa Gor Mahia Kenneth Muguna ametoa changamoto kwa wachezaji wenzake kuimarisha fomu yao barani Afrika.

Mabingwa hao wanajitayarisha kusafiri hadi Algeria kuchuana na USM Algers katika mkondo wa kwanza ya ligi ya Caf Champions siku ya Jumapili.

Safari za K’Ogalo za dakika ya mwisho, zimekua zikiathiri matayarisho yao.