RONGO: Polisi wanasa bhangi yenye thamana ya Sh20,000 eneo la Kanga

Mtu mmoja anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Rongo baada ya kupatikana na bangi yenye thamani ya Ksh20, 000.
Kulingana na kamanda wa polisi wa Rongo Bw.David Ngetich alisema kuwa Jamaa huyo kwa jina Evance Odhiambo mwenye umri wa miaka 28 wakiwa wawili kwenye pikipiki  lenye sajili ya nambari KMDM 511Y kuelekea upande wa Kisii alifumaniwa hiyo jana mchana na maafisa wa polisi mjini Rongo waliokuwa katika maziara zao mjini humo na kuwashuku mienedo zao. 
“Maafisa wetu walitoka kwenye kituo cha petroli ndipo  wakaweza kuona majamaa wawili wakitorokea upande wa Migori kuelekea Kisii na godoro kimechakaa  kwenye pikipiki ndipo wakawashuku na kuanza kuwafuata kabla ya kushikwa eneo la Sare Kamagambo,”alieleza Ng’etich.
Ngetich aidha alisema kuwa jamaa mmoja aliweza kuchana mbuga kuepa vizwizi vya polisi waliokuwa wakiwafuata na kupatikana na jumla ya misokoto 200 ya bangi.
Kamanda huyo wa polisi alikiri kuwa matumizi na biashara ya bangi inaongezeka katika eneo hilo jambo ambalo alisema kuwa kama maafisa wa usalama watafanya kile wawesalo kukabilianalo akisema  imeharibu watu wengi hasa vijana ambao wanastahili kusaidia jamii kimaendeleo na hoja dhabiti ya kujiimarika kimaisha.
Alisema kuwa maafisa wa polisi kwa ushirikiano na umma wataendelea kushika doria na kuhakikisha kuwa biashara hiyo haramu inakabiliwa nalo katika eneo hilo.
Hata hivyo alihimiza wakaazi wa eneo hilo kumsadia kukabiliana na biashara hiyo haramu ambao umeanza kukithiri katika eneo hilo akisema vijana wengi kwa sasa wameanza kutumia madawa hizo mbali na kujiunga na vikundi hatari vya uwizi.
Alisema kuwa maafisa wa polisi wataendela kufanya kazi pamoja na wakaazi hao kukabiliana nalo akitoa wito kwa viongozi na wadau mbalimbali katika eneo hilo kutafuta namna mwafaka ya kukabiliana na ongezeko la matumizi ya bangi katika eneo hilo hasa dhidi ya  vijana.
Mshukiwa huyo atafikishwa kortini Rongo hapo kesho kujibu mashtaka dhidi yake.