Rose Muhando aanza kuimba tena.

unnamed (2)
unnamed (2)
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Rose Muhando, aliushangaza umati alipokuwa akitumbuiza huko nchini Tanzania alipowasimulia maisha yake ya hapo awali.

Rose Muhando aliwaacha mashibiki wakibubujikwa na machozi baada ya kuimba wimbo wake maarufu 'Ndivyo Ulivyo.'

 "Sikuwahi fikiria ningekuwa natumbuiza umati huu wakati kama huu lakini kwa neema na mapenzi yake Mwenyezi Mungu ameniwezesha kuwa hapa," Rose alisema.
Mara ya mwisho Rose kuonekana hadharani, ni wakati alikuwa akitoka hospitalini baada ya kulazwa kwa muda mrefu.

Picha yake akiwa amerejelea hali yake nzuri ya kiafya ilichapishwa kwa mtandao na mwimbaji wenzake Betty Bayo.