Rubani jasiri anusuru maisha ya abiria ndege ilipopigwa na radi angani

WhatsApp Image 2019-11-27 at 12.36.13 (1)
WhatsApp Image 2019-11-27 at 12.36.13 (1)
Rubani aliyefanikiwa kutua salama pamoja na abiria wote 41 licha ya ndege hiyo kupigwa na radi na kuharibika vibaya amepongezwa.

Picha za ndege hiyo aina ya Proflight DHC-8-300 zimesambaa mtandaoni na ilikuwa inapaa kutoka Livingstone ikielekea jiji kuu la Zambia, Lusaka ilipopigwa na radi.

Kulikuwa na mvua nyingi sana na radi ikapiga sehemu ya mbele ya ndege hiyo na kuiharibu kabisa.

Ndege hiyo ilikuwa inapaa angani futi 19000 hali hiyo hatari ilipotokea.

Abiria mmoja aliyekuwa akisafiria ndege hiyo alisema kuwa: " Ndege yetu iliathiriwa na mvua kubwa iliokuwa inanyesha, na tulipokaribia kutua, tukasikia mngurumo wa radi. Tulishtuka sana, lakini baada ya dakika chache tulifika eneo salama."

Abiria pamoja na watumizi wa mtandao wengi waliziona picha hizo wanatoa wito kwa rubani wa ndege hiyo atuzwe.

"Ninashukuru juhudi za rubani huyo hodari, ameokoa maisha ya wengi, ameonyesha utaalamu wa hali ya juu." mwengine alisema.