"Rudisha mama ama utafute mtu!" Jaguar amshawishi Eric Omondi

eric-omondi
eric-omondi
Mheshimiwa Charles 'Jaguar' Njagua amemsuta mcheshi na msanii Eric Omondi kumrudisha aliyekuwa mpenziwe, bi Chantal maishani mwake.

Kupitia kwa kanda iliyochapishwa katika mtandao wa Eric Omondi, Jaguar ambaye alikuwa ameenda kumtembelea rafikiye kwake nyumbani.

Akiwa humo, aliandaliwa staftahi na inaonekana hakuridhishwa na hapo akamrai Omondi amrudishe Chantal.

Omondi na Chantal walitengana mwaka huu mwezi wa Mei alipotangaza kuwa njia zilizowaleta wapendwa hao wawili, ziliwapa mielekeo tofauti.

Aliandika,

As you move into your new phase in life with or without me I want to wish you all the best My Love❤️…The paths that brought us together are now facing different directions. The post read in part.

Ingawa Jaguar alishukuru juhudi za Omondi kumuandalia chai, anahisi kuwa ni muhimu amrudisha chantal au hilo likishindikana, basi atafute mpenzi mwingine kwani wako wengi zaidi.
Soma jinsi mazungumzo yao yalivyokuwa;

Jaguar: Rudisha mama

Eric Omondi: Chai ilikuwaje bila mama?

Jaguar: Chai haiko lakini ahsante kwa breakfast, lakini tunaomba urudishe mama. Hata wewe sasa utanona, utaongeza weight ama utafute mtu, watu ni wengi.

Eric Omondi: Nitafute mtu ama mama arudi?

Jaguar: Mama arudi au utafute mtu

Tazama kanda hiyo

https://www.instagram.com/p/B3G0EJwAhXD/