Hii ni kwa sababu Ruth alisema kuwa mumewe alimshauri asiweze kusema chochote kwa familia kuhusu kulazwa kwake hospitalini
Mumewe Matete aliaga dunia kwa ajili ya mejeraha aliyopata kwa ajili ya mlipuko wa gesi nyumbani kwao
Ruth alihojiwa na wapelelezi wa DCI na aliwaeleza kuhusu mazungumzo ya mwisho na mumewe kuhusiana na jinsi alivyomzuia asiseme lolote kuhusu kulazwa kwake hospitalini .
Kulingana na wakili wa Ruth Matete, mumewe alimsihi asiwaambie jamaa zake kuwa yupo hospitalini na asijaribu kuwaambia kuhusu ajali ya mlipuko wa gesi nyumbani kwao
“HE REQUESTED HER NOT TO TELL HIS FAMILY WHAT HAPPENED BECAUSE HE DID NOT WANT THEM TO GET WORRIED. IN HIS FIRST WEEK IN HOSPITAL, HE VIDEO CALLED HIS BROTHER TO ASSURE THE FAMILY THAT HE WAS ON THE ROAD TO RECOVERY. THAT WAS BEFORE HIS WOUNDS BECAME SEPTIC AND HIS KIDNEYS STARTED FAILING." Alizungumza wakili.
Wakili wake alisema kuwa Ruth aliwaarifu jamaa za John kuwa yupo hospitalini kwa ajili ya kidonda cha tumbo kwa lugha ya kimombo 'appendicitis'.
“THEY WERE APTLY INFORMED WHEN HE DIED."
Mara ya kwanza familia yake ilikuwa na shida kwa kutoambiwa ukweli lakini walipoelezewa na wakili wa Ruth kilichojiri walielewa.
Afisa wa DCI kutoka Athi river Vincent Korir alizungumza na kusema hamna mashtaka yoyote yatakayopendekezwa dhidi ya Matete na wanangoja ripoti ya upasuaji wa mwili wa mwendazake .