Ruto ajitetea kuhusu kauli ya "Kutangatanga". Asema yupo kufanya maendeleo

unnamed__7___1567930725_82823
unnamed__7___1567930725_82823
Naibu wa rais William Ruto sasa anahoji kwamba juhudi zinazowekwa kuibadilisha katiba hazipaswi kamwe kuwa kisiki kamwe katika mipango ya maendeleo ya serikali .

Ruto amesema kwamba nchi hii haiwezi kubadilishwa kupitia mageuzi ya katiba ila ni kuidhinisha mipango ya maendeleo katika sehemu mbalimbali nchini.

Akizungumza katika ziara ya kukagua miradi kaunti ya Vihiga hapo jumamosi, Naibu wa Rais alisema miito ya mara kwa mara kuifanyia marekebisho katiba haiwezi kuingilia utendakazi na ajenda ya Jubilee.

Soma hadithi hii hapa;

"Maendeleo hayatasitishwa na siasa zinazofanyika za kubadilisha katiba. Wakenya wanataka miundomisingi kama barabra,hospitali,shule, bima za afya za hpospitali na nyinginezo ili waboreshe maisha yao na wala sio siasa." Ruto

Waliokuwepo katika ziara hiyo ya naibu wa rais ni Charles Gimose (Hamisi), Benjamin Washiali (Mumias mashariki), John Waluke (Sirisia), na aliyekuwa gavana wa Vihiga Moses Akaranga na Boni Khalwale.

Ruto alisema kuwa Jubilee ipo tayari kufanya kazi na kiongozi yeyote bila kujali mrengo anaoegemea wa kisiasa akihoji kuwa huu sio wakati wa siasa.

Soma hadithi hii hapa;

Ruto alisema kuwa viongozi wasishangae kuona akitanga sana nchini.

"Haijalishi ni nani ananialika katika mikutano ya maendeleo kwa sababu ajenda yetu ni kuhudumia wakenya. Ziara zangu nchini sio za kufanya siasa. Kuna wakati wa kila jambo." William Ruto.