Ruto aonyesha dalili za wasiwasi, amtaja Raila Odinga Embu

Naibu wa Rais William Ruto sasa anaonyesha dalili za kuwa huenda Raila Odinga anabania nia yake ya kuwa rais wa Kenya.

Katika ziara ya jana kaunti ya Embu, Ruto alionyesha wasiwasi mkubwa kuwa huenda Raila ana njama ya kuvunja chama cha Jubilee.

Ila je? Mbona ni Ruto peke yake na wandani wake walio na wasiwasi huu?

Soma hadithi nyingine;

 Ruto alimuonya aliyekuwa waziri mkuu na kinara wa ODM Raila Odinga kujiepusha na siasa za chama cha Jubilee.

William Ruto ametoa taarifa kwamba Raila ana nia ya kuvuruga chama hiki.

Aidha Ruto amemtaka Raila kumakinika katika maswala ya chama chake cha ODM.

Kulingana na Ruto, chama cha ODM kina matatizo tele ambayo yanafaa kuangaziwa.

"Huyu mtu wa Vitendawili anajaribu kubomoa Jubilee. Anadhani kuwa akifanya hivyo atapata uongozi. Nataka nimwambie kuwa Jubilee imejengwa katika misingi imara na hatatoboa kuibwaga." Alisema William Ruto.

Ruto alisema haya katika kaunti ya Embu kijiji cha Kabaci alipokuwa akifungua ujenzi wa chuo cha kiufundi cha Siakago.

Ujenzi wa chuo hiki unadhamiriwa kugharimu shilingi milioni 100.

Soma hadithi nyingine;

Ruto alisisitiza kuwa Jubilee ipo imara na Raila hawezi kuigawanya katu.

Naibu wa rais alionyesha ghadhabu kuwa Odinga anawapa mwelekeo wa jinsi ya kuendesha chama cha Jubilee.

"Ni jambo la ajabu mtu wa vitendawili anatufunza jinsi ya kuendesha chama wakati nyumba yake ya ODM ina nyufa."

Huku akimwonyesha Raila kama kiongozi asiye na mwelekeo, Ruto alisema kuwa wakenya wazidi kumwombea.

Raila Odinga hajamjibu kufikia sasa.

Soma hadithi nyingine;

Ruto anaonekana kuwa na machungu na kiongozi wa ODM kuliko mtu yeyote katika chama cha Jubilee.

Je, huenda ikawa Raila anabana ndoto ya Ruto kuwa Rais wa Kenya?
Wabunge wa eneo hilo Geoffrey King'ang'i (Mbeere Kusini) Eric Muchangi (Runyenjes),Muriuki Njagagua (Mbeere Kaskazini), John Muchiri (Manyatta),  Kimani Ichung'wa (Kikuyu) na Cecily Mbarire walimpa hakikisho kuwa hawatakubali Raila kuleta wasiwasi katika chama cha Jubilee.