Ruto apuuza agizo la Uhuru kuhusu ukaguzi wa miradi

Naibu rais William Ruto siku ya Jumapili alisema kwamba ataendelea kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuzindua miradi katika kile kilichooenekana kama kukaidi agizo la rais.

Akiwa zaiarani katika maeneo yam lima Kenya Rais Kenyatta alitangza kwamba yeye mwenyewe atakuwa akigaua miradi ya maendeleo. Lakini akizungumza katika eneo la Itiero katika hafla ya kutawazwa kwa Askofu Joseph Omwoyo wa kanisa la Lutheran kanda ya Kusini magharibi mwa Kenya, Ruto alisema kwamba hataogopa kuzungumzia miradi ya maendeleo.

Huku akionekana kumkosoa kinara wa ODM Raila Odinga, Ruto alisema kwamba “wakenya sio wajinga, kufuata hadidhi na fitina”

Alisema wakenya wamejanjaruka kuliko awali kufanya maamuzi muhimu kuhusu viongozi wanaowaka.

Naibu Rais alisema kwamba majukumu yake yanajumuisha kuzungumzia mambo ambayo serikali imefanyia wakenya.

Akiwa Kisii Ruto alisema kwamba miradi mingi ya miundo msingi tayari imekaribia kukamilika huku mingine mingi ikiwa tayari imekamilika. Ruto alikosoa wanasiasa wanao kashifu wanasiasa wanaoegemea mrengo wake akisema kwamba ajenda kuu ya BBI ni kuunganisha wakenya na wala sio kutenganisha taif

“ikiwa tunajenga daraja la kuunganisha wakenya, tufanye hivyo bila kuwa na nia fiche. Daraja hujengwa kuunganisha na sio kugawanya wakenya”.

BBI inawapa wakenya nafasi kuzungumza na kila mmoja, naibu rais alisema.