Ruto avunja kimya kirefu kuhusu mkutano wa Gema Sagana

unnamed
unnamed
Hatimaye Ruto amevunja ukimya wake kuhusiana na mkutano wa Gema uliofanyika Ijumaa.

Katika mkutano huo,Uhuru aliwaonya wanaopinga BBI na kuwahimiza viongozi wa mlima Kenya kuunga mkono 'Handshake'

Uhuru alisema tayari matunda ya BBI yalionekana katika uchaguzi mdogo wa Kibra wa Novemba 7.

“Katika miaka yangu yote sijawahi ona kampeni ya amani Kibra. Kuna baadhi ya watu wachache walirushiwa mawe lakini hatukuona duka likichomwa au watu wakiwa na wakati mgumu wakienda nyumbani,” Uhuru alisema.

“Iwapo uchaguzi unaweza ukafanywa Kibra na watu hawatapoteza mali yao au maisha yao basi hiyo ni ushindi na watu wanafaa kujifunza kutokana na hilo.” Uhuru.

Ruto ambaye amekuwa mnyamavu kuhusiana na matukio ya kisiasa yaliyofanyika Sagana ameamua kutoa wazo lake.

Kupitia mtandao wa Twitter, Ruto amesema kuwa mkutano wa Ijumaa Sagana uliziba nyufa na kukifanya chama imara zaidi.

Haya yanajiri huku chama cha ODM kikimsifia sana Rais Uhuru Kenyatta kuhusu tamko la lengo la BBI katika mkutano uliofanyika Sagana.

Aidha, mwenyekiti wa ODM amesema kuwa Uhuru anathamini sana ‘Handshake’ iliyofanyika kati ya Raila Odinga na Uhuru Kenyatta.

Mengi yanasubiriwa kufanyika katika ulingo wa kisiasa tukisubiri mwaka wa 2022.