Ruto hachelei! amrejeshea Raila makombora ya siasa za katiba

Naibu Rais William Ruto siku ya Jumanne alipuuzilia mbali matamshi ya kinara wa upinzalni Raila Odinga akidai kwamba Raila alikuwa akitumia mjadala wa kura ya maoni kutawanya wakenya.

Aliwataka wakenya kuwapuuzilia mbali viongozi wanaotaka kutumia mwito wa kubadilisha katiba kama njia ya kuligawanya taifa, kuleta uhasama na kuzua hali ya swintofahamu nchini.   Akihutubia wananchi nje ya Hospitali ya Rufaa ya Kapsabeut, Ruto alisema kwamba Jubilee haitamruhusu mtu yeyote kugawanya wananchi kwa manufaa yake ya kibinafsi.

“Baadhi ya viongozi wanafaa kuacha kutuhadaa na vitisho. Hatutakupa nafasi kugawanya taifa,”alisema. Aliongeza, “Wakati BBI itawasilisha mapendekezo yake, tutayajadili kwa utaratibu. Hatutakubali uchochezi wa Tsunani unotawanya taifa hili tena,” Ruto alisema.

Kinara wa upinzani Raila Odinga siku ya Jumapili alionya kwamba Ruto na kikundi chake cha Tangatanga watafagiliwa hadi ghala la sahau la siasa. Siku ya Jumamosi, Rais Uhuru Kenyatta alionekana kuunga mkono mabadiliko ya katiba huku jopo la BBI likitayarisha ripoti yake ya mwisho.

“Kama kuna kitu hakifai katika katiba, au sheria yoyote ile,tunahitaji kukaa chini na kuona njia mwafaka kurekebisha makosa,” Rais Kenyatta alisemasiku ya Jumamosi. Siku ya Jumanne Ruto alisema maswala ya katiba ni mazito na yanafaa kuhusisha wakenya wote.

“Tunataka kuhakikisha kwamba kama taifa, chochote kitakacho pendekezwa, katika mfumo wowote ule, hakionyeshi kwamba kuna upande wa washindi na waliopoteza,” Ruto alisema.