Ruto ni rafiki wa zama kabla niwe waziri-Echesa

Aliyekuwa waziri wa michezo Rashid Echesa alikiri kuwa naibu wa rais William Ruto ni rafiki yake hata kabla awe waziri wa michezo.

Aliongeza na kusema kuwa haitaji wakala wowote anapoenda  kumtembelea naibu wa rais.

Echesa aliongea baada ya kukamatwa na kumaliza wiki moja kizuizini, aliachiliwa kwa dhamana ya millioni moja.

Ruto alikataa madai hayo, kuwa Echesa hakuwa na wakala wowote alipomtembelea katika ofisi yake eneo la jumba la Harambee kuhusu mpango wa kushughulikia vifaa vya kijeshi bandia.

Echesa aliwaarifu askari wanaolinda afisi ya Ruto kuwa ana wakala na naibu wa rais jambo ambalo Ruto alikana baadaye.

Akiongea katika mahojiano na runinga ya NTV, Echesa alisema kuwa yeye na naibu wa rais ni marafiki wa muda mrefu hata kabla ya awe waziri.

"Si hitaji wakala wowote ili kumuona naibu wa rais Ruto, kwa sababu sisi ni marafiki kutoka kitambo, wacha wapeleke ushahidi mbele ya mahakam." Echesa Alisema.

Alikana madai ya kusaini mkataba wa kushughulikia vifaa vya kijeshi huku akisema hajui billioni 40 zimetoka wapi na kwa nia gani.

"Sijui billioni 40 kwenye zilitoka, sijawahi tia saini katika mkataba wowote na kama nilitia basi sheria hiko na pia iko wazi.

Nataka kumpa DCI changamoto achapishe saini hizo." Alizungumza Echesa.

Alizidi na kuonea na kusema kuwa  Stanley Kozlowski, ambaye ni mkuu katika madai ya kashfa hiyo amekuwa rafiki yake kwa muda wa miaka sita.

" Mama yake ananijua sana, mama yangu na baba yangu wanamjua Stan alikuja huku kwa ajili ya utalii."

Sikujua kuwa alikuwa na biashara humu ambacho nili jua hakuwa na kibali cha kufanya kazi."Alisema.

Echesa alisema kuwa hajawahi kuwa na kampuni wala si mkurugenzi wa kampuni yeyote.

Cha mno walishtakiwa kwa kumlaghai Stanley mabillioni za pesa huku wakimwambia uwa watampa vifaa vya kijeshi ili auze.

Echesa alikataa madai hayo yote.