Sababu 5 mbona familia ndizo zitafaidika wakati huu wa curfew

Kuna vile nahisi kuwa tangia visa hivi vya Corona kuchipuka nchini, nimekuwa nikiangazia mambo kwa njia isiyokuwa ya kuleta raha  kwani ugonjwa huu umeleta woga na maafa mengi kuliko habari njema.

Hata hivyo, huku nchi nzima ikiendelea kuzingatia curfew ambayo huwezesha wakenya kuwa kwa nyumba kuanzia mida ya saa moja joi hadi saa kumi na moja asubuhi, nahisi kuwa familia ndizo zitafaidika zaidi katika hali hii.

Nimeorodhesha sababu tao ambazo nahisi kuwa familia zitasaidika wakti huu wa curfew na kwarantini kuliko watu wengine duniani.

Mda wa kutosha na familia

Hili hata bila ya kuelezea zaidi, linaelezea jinsi mambo yalivyo katika vyumba vingi sasa hivi. Familia nyingi kwa sasa zinafurahia kutebea pamoja kila jioni, kucheza michezo kadha wa kadha,kupika pamoja na pia mambo mengi ambayo huleta wapendwa pamoja.

Haya basi yatasaidia kuwezesha familia nyingi kuwa na upendo mwingi na kuwa na umoja kwa siku za usoni.

Kuhakikisha kuwa umejua talanta za mwanao

Kusema kweli, baba wengi huwa hawafahamu talanta za wanao kwani mara kwa mara huwa mbali na nyumbani na ni wake zao ambao huwa na bahati ya kuzitambua talanta za wanao wakiwa wadogo.

Hali hii yote itawapa kina baba nafasi murwa ya kuzitambu na kuzifanyia kazi talanta za wanao kwani hawana chaguo ila kuwa nao kila wakati.

Mafunzo ya nyumbani

Wazazi pia watachukua firsa hii kuweza kuwafunza wanao nyumbani na ni katika harakati hii ambapo wataweza kujua masomo ambayo watatilia maanani zaidi kuliko mengine na hili litasaidia kuwaleta wazazi na wana wao pamoja na kuboresha uhusiano wao zaidi.

Kuwaelimisha zaidi kuhusu maadili ya mungu 

Kuanzia zama zama za kale, familia zote zikiongozwa na mzee wa nyumba au mama wa nyumbani, lazima kuwe na mafunzo kuhusu maadili mema na umuhimu wa kumtegemea mola.

Basi wakti huu utakuwa bora kwa familia ambazo zimepoteza maadili mema ya mwenyezi mungu, kwa mfano kuomba pamoja, kusoma biblia na jinsi ya kuweka imani yote kwa mungu.

Wapenzi kuboresha uhusiano wao

Watoto kando, mda huu wote waweza kuwa tu kile ambacho wapenzi wengi au wazazi weni wamekuwa wakitamani. Kwa mfano,wazazi wengi hupatana tu wikendi na kuwa na wakati wa kutosha pamoja na sasa wana fursa ya kupanga mikakati yao bila kusumbuana na yeyote na bila haraka kamwe.

Hili litawasaidi kuzidisha mapenzi yao na kusaidia kujenga familia yao kwa misingi ya upendo.