Sababu ya kuanzisha na vile nilianzisha timu ya mpira ya Majirani FC - Majirani

Katika kilele cha mgawanyiko wa kitaifa wakati wa uchaguzi wa 2017, msanii (rapper) Majirani aliweza kuanzisha timu ya mpira inayoitwa Majirani FC katika kaunti ya Eldoret.

Alisema kuwa mpira wa kandanda ndio tu ungeweza kuunganisha watu katika makabila yote.

"Imekuwa miaka miwili tangu nifanye miradi yangu, kwa sababu ta changamoto, na pia shauku ya klabu,

"Nataka klabu hicho cha kandanda kuwa imara ili niweze kurudi katika sekta ya usanii," Alizungumza Majirani.

Majirani aliwashauri vijana waweze kuleta mawazo mapya na pia kuyatumia ili kuwasaidia wenzao.