Sababu za kumpenda Diamond Platnumz - Lilian Muli

Mtangazaji wa runinga ya Citizen Lilian Muli ameweza kufungua moyo wake na kufichua kwanini anapenda muziki ama nyimbo za Tanzania. Aliweza kusema akiwa katika mahojiano ya Malkia Afriza Production.

Lilian aliongezea na kusema kuwa waimbaji wa Tanzania ni wenye mapenzi tele.

Kusema au kufichua kwake mtangazaji Lilian upendo wake usioisha kwa ajili ya muziki ama nyimbo za Tanzania kunakucha tu baada ya wasanii wa Kenya kudai na kukampeni nyimbo zao ziweze kuchezwa katika vyombo vya habari kupitia #PlayKenyanMusic.

Kabla sijatia kikomo katika makala haya mtangazaji huyo pia aliweza kujuta kwa kumuita baba ya mtoto wake mume wa jamii.

Hii ni baada ya wananchi kuweza kumuongea kwa sana katika mitandao ya kijamii.

"Katika  usemi wangu wa awali, ulikuwa wakati wangu ambao nilikuwa chini au mgumu, na pia sina kiburi na usemi huo kwa maana ilifanya wananchi kuongea kunihusu na pia 'Diaspora'," Lilian aliongeza.

Alisema pia aliweza kusoma funzo kupitia makosa yake ya awali, pia aliweza kukiri kuwa ulikuwa wakati wake ambao ulikuwa mgumu katika maisha yake na ameweza kutatua  kila kitu na tayari ameendelea na maisha yake.