Sack Him! Baadhi ya wabunge wa Jubilee wataka Duale atimuliwe

Wabunge 117 wa chama cha Jubilee sasa wanamtaka kiongozi wa chama hicho rais Uhuru Kenyatta kumfurusha mbunge wa Garissa mjini Aden Duale kutoka kwa kiti cha kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa.

Mrengo wa kieleweke ambao ni mojawapo wa wabunge wa Jubilee walikasirishwa na hatua ya Duale kuendelea kuwa kiongozi wa wengi katika bunge hilo huku wenzake ambao walikuwa waasi wakitimuliwa kutoka kwa nyadhifa zao.

Kutokana na hatua ya rais Kenyatta kukosa kumtimua Duale kutoka kwa wadhifa wake, sasa wabunge hao wameanza mchakato wa kuchukua saini za kutaka kumfurusha kutoka kwa wadhifa huo.

Duale kwa upande wake amesema viongozi hao walishindwa kuwasilisha pendekezo hilo wakati wa mkutano wa chama hicho kwenye Ikulu jijini Nairobi.

“I am used to Kanini Kega’s petitions. He brought two against me in the 11th Parliament but they both flopped. He needs to acquaint himself with the preocedures for appointing and removing parliamentary leaders in accordance with the law,”  amesema Duale.

Mrengo huo wa Kieleweke sasa unasema rais Kenyatta hakupendekeza Duale kusalia katika uongozi wake wakati ambapo rais Kenyatta alikuwa anasoma majina ya watu waliokuwa wanastahili kuendelea katika nyadhifa zao.