Court

SAD:Mvulana mwenye umri wa miaka 11 amuua kakake wakipigania chaja ya simu

Mvulana amwenye umri wa miaka  11 aliyemuua  kakake kwa kumdunga kisu wakipigania chaja ya simu atazuiliwa katika rumande ya watoto kwa siku tatu ,mahakama ya Nakuru imeagiza. Upande wa mashtaka umetaka kupewa muda kushauriana iwapo mwanafunzi huyo wa darasa la tano anafaa kushtakiwa .

CRIMINAL or VICTIM? Ufichuzi watolewa kuhusu mwalimu aliyeuawa na mwili wake kuchomwa Kitui .

Polisi wanashikilia kwamba mtoto huyo lazima ashtakiwe lakini mawakili wake  wanasema  kesi hiyo inafaa kutupiliwa mbali kwa msingi kwamba hawezi kushtakiwa  kwa sababu ya umri wake mdogo .  Wakili wake anasema kwa mujibu wa sheria  mtu aliye chini ya umri wa miaka 12  hana uwezo wa kutekeleza uhalifu givyo basi  mtoto hakujua iwapo ni hatia kumwua kakake .

5th President: Mmoja kati ya mafahali hawa huenda akawa rais wa Tano wa Kenya .

Mtoto huyo atazuiliwa katika   rumande ya Nakuru Children’s Home   huku mahakama ikingoja ripoti  ya kuamua hatua itakayofuata . Mtoto huyo anadaiwa kumuua kakake mwenye umri wa miaka 15  disemba tarehe 31 mwaka jana  katika viunga  vya mji wa Nakuru .Wawili hao walianza kulumbana wakati mshukiwa alipoitoa chaja kutoka kwa rununu ya kakake . majirani wanasema wazazi wao walikuwa wamesafiri mashambani kwa sherehe za krisimasi na kuwaacha watoto hao chini ya utunzi wa mjomba yao.mahakama itatoa uamuzi wa iwapo itamshtaki mvulana huyo  januari tarehe 16 mwaka huu .

Photo Credits: radio jambo

Read More:

Comments

comments