Safari ya Gor kuelekea Algeria huenda ikatatizwa na ukosefu wa hela

Safari ya Gor Mahia kueleka Algeria kwa mechi ya CAF Champions League dhidi ya USM Alger iko katika utata baada ya klabu hio kukosa fedha za kutosha.

Mwenyekiti Ambrose Rachier anasema hawakupata pesa za kutosha kutoka kwa mchango ulioandaliwa Jumanne.

Gor wamepangiwa kupambana na USM Alger katika mechi hiyo ya mkondo wa kwanza wa michuano hiyo siku ya jumapili.

Tukielekea bara Ulaya, ajenti wa Jadon Sancho alikutana na maafisa wa Manchester United wakati wa dirisha la uhamisho la msimu wa joto, kulingana na mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc.

Sancho amehusishwa na United na vilevile vilabu vingine vya Uropa kufuatia misimu miwili ya kufana akiwa Dortmund, ambapo alifunga mabao 17 na kusaidia mara 27 katika mechi 60.

Dortmund inasema ilikataa ofa ya kumtaka mchezaji huyo kutoka kwa klabu moja kubwa mapema mwaka huu.

Arsenal inasema hakuna wachezaji wowote wa kimataifa wameripoti majeraha licha ya kiungo wa kati Lucas Torreira kutolewa nje ya mechi ya Uruguay waliyotoka sare na Marekani akiwa na tatizo la msuli.

Timu hio ya Marekani Kusini ilithibitisha kua kutokana na tatizo hilo, Torraeira hakucheza mechi yao waliyotoka sare ya 1-1 huko St Louis Jumanne usiku.

Kiungo Nicolas Pepe pia hana jeraha. Arsenal pia imethibitisha kua mlinzi Rob Holding ameregelea mazoezi kutoka kwa tatizo lake la goti la muda mrefu.

Real Madrid na Chelsea wamekubaliana mkataba wa uhamisho wa mchezaji N’Golo Kante kulingana ripoti. Raia huyo wa Ufaransa alikua amfuate Eden Hazard Bernabeu wakati wa dirisha la uhamisho msimu wa joto, lakini akaamua kusalia Stamford Bridge kwa miezi 12.

Hii ilikua pigo kwa meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane, ambaye alikua na hamu ya kumsajili mchezaji huyo  La Liga.

Chelsea pia wanaripotiwa kukubali Real Madrid kuwaarifu iwapo watataka kumuuza Kante.