Safaricom yajibu KRA, akaunti zote M-Pesa zitafunguliwa?

unnamed (1)
unnamed (1)
Kampuni inayoongoza Afrika Mashariki Safaricom imetoa kauli baada ya mamlaka ya kutoza kodi KRA kutangaza kuchunguza akaunti za wateja wake.

Safaricom sasa ipo tayari kwa kufungua akaunti zote za M_pesa iwapo uchunguzi huo utafuata sheria.

Kampuni ya Bolt imesema kuwa ipo tayari kuenda sawa na mapendekezo watakayotoa KRA.

Mamlaka hii ya kukusanya kodi ilitangaza mpango wa kuwanasa wanaokwepa kulipa kodi kupitia mifumo ya kidigitali na M-Pesa.

Soma hadithi nyingine:

KRA pia itachunguza kila operesheni ya hela katika PesaLink, PayPal na mifumo mingine ya kutuma na kupokea hela.

KRA zaidi ya hapo inazitaka kampuni zinazofanya kiditali kama Facebook, Twitter na Uber zilipe kodi hapa nchini.

Maafisa wa KRA katika mahojiano wamedokeza kwamba wapo na habari za uwepo wa biashara nchini zinazoendesha kidigitali na kupata pato kubwa katika mitandao.

Soma hadithi nyingine:

Joseline Ogai, ambaye ni makamu wa kamishna katika kitengo cha utafiti, ukusanyaji habari na mipango akiwa na Maurice Orei ambaye ni makamu wa kamishna wa sera katika mamlaka ya  KRA wnasema kuwa juhudi za kusawazisha data zimeanzishwa.

Katika mahojiano ya kina ndani ya mjengo wa ghorofa Times Towers, maafisa hawa walidokeza kuwa mpango na utaratibu wa kusawazisha data utasaidia pakubwa kuchunguza mapengo yanayojitokeza katika ulipaji kodi.

Soma hadithi nyingine:

“Tunachukulia utaratibu huu wa kusawazisha data kwa umakini zaidi katika juhudi za kuchunguza ulipaji kodi katika mifumo ya kidijitali. Muda usio mrefu tutawanasa wanaokwepa kulipa kodi ila pesa wanayotengeza katika mitandao ni nyingi mno.” Alisema Ogai

Soma hadithi nyingine:

“Huwezi kuwa unalipa kodi kiasi cha chini ila pesa unayoingiza katika M-Pesa inayotokana na haso za kikando iko juu zaidi na hausemi.” Alisema Ogai.

Wawili hawa walisema kuwa hii ni njia nzuri ya kutumia ukizingatia kuwa sekta hii inazidi kupanuka na njia zilizopo za kawaida za ulipaji kodi zinavuja.