Safaricom yakana madai ya udukuzi huku ikiomba walionufaika na data, muda wa maongezi kurejesha

Bamba 100
Bamba 100
Kulikuwa na sintofahamu Jumatano baada ya madai  kuibuka kwamba mitambo ya safaricom ilidukuliwa na mtu asiyejulikana na kuruhusu wateja kunufaika na data pamoja na muda wa maongezi wa bwerere inayogharimu mamilioni ya pesa.

Ripoti ambazo hazikuthibitishwa zilisema kwamba  mdukuzi huyo alidukua mfumo wa mitambo ya Safaricom na kuwaruhusu  wateja kunufaika na  idadi ya kubwa ya  data bila malipo.

Inasemekana kampuni hiyo ilipata hasara ya data ya thamani ya  kima cha shilingi milioni 500 na muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi 1 milioni.

Hata baada ya polisi kusema wamemkamata mhusika, Safaricom ilitupilia mbali madai hayo na kusema ni uvumi tu.

Safaricom inawaomba  wale ambao walijipatia data na muda wa maongezi bila malipo na kinyume  cha sheria  kufika katika maduka yao ya karibu ili kurekebisha makosa hayo.

Kamishna wa kaunti ya Kiambu Wilson Wanyanga alisema maafisa wamemkamata mtuhumiwa huyo huko Juja na jamaa huyo atafikishwa  mahakamani Alhamisi. Aliwaambia waandishi wa habari mtuhumiwa huyo  alikamatwa na kadi za safaricom  1,000 za Simu.

Wanyanga alisema mtuhumiwa huyo, anaamika  kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu, alidukua mfumo wa mtambo wa Safaricom na kuruhusu wateja kupata bidha hizo muhimu ambazo huwa ndiyo pato kubwa sana kwa kampuni hiyo.

Safaricom, hata hivyo, walikanusha kuwa hawakujua madai hayo. Meneja wa mawasiliano ambaye  hakutaka jina lake liwekwe wazi alisema kwamba  polisi walikuwa wamekamata watu wengi ambao wanatekeleza uhalifu wa kubadilisha kadi za simu na kuibia watu pesa kutoka M-Pesa.

"Hatujui kuhusu ya utapeli wa aina hii. Hatuna habari kuhusu kukamatwa kwa mtu yeyote aliyehusika. Tunachojua ni kwamba polisi wamekuwa macho kwa wabadilishanaji haramu wa kadi za simu na na watapeli wa M-Pesa. "alisema.