Safaricom yamteua afisa mkuu mtendaji

ndegwa
ndegwa
Peter Ndegwa ameteuliwa kuwa afisa mkuu mtendaji katika kampuni ya Safaricom.

Bodi ya wakurugenzi ya Safaricom ilisema katika taarifa siku ya alhamisi kwamba Ndegwa ataanza kazi rasmi Aprili tarehe moja 2020.

Ndegwa amejiunga na Safaricom kutoka kampuni linalofahamika kama Diageo ambapo yeye ni mkurugenzi mtendaji wa Diageo Bara Ulaya.

 Mwenyekiti katika kampuni ya Safaricom Nicholas Ng'ang'a alisema kuwa Ndegwa ana uzoefu mwingi katika usimamizi, mikakati ya kibiashara, na uendeshaji wa fedha kwani amefanya kazi hilo kwa muda wa miaka 25 katika majukumu mbalimbali ndani ya sekta ya huduma za kifedha.

Ndegwa atachukua nafasi ya Michael Joseph ambaye alihudumu kama afisa mkuu baada ya kufariki kwa Bob Collymore.

Collymore aliaga dunia mnamo juni mwaka huu baada ya pigano kali na ugonjwa wa saratani.

Taarifa kutoka kampuni hiyo ya mawasiliano ina matumaini kuwa Ndegwa atachangia pakubwa kubadilisha maisha katika jamii.

Safaricom inamilikiwa na Vodacom ya Afrika Kusini kwa asilimia 35%, serikali ya Kenya ina hisa asilimia 35%, asilimia 25% inauzwa katika soko la usalama la Nairobi, huku Vodafone group ina hisa ya asilimia 5%.

Safaricom inadhibiti takriban asilima 62% ya soko ya rununu ya Kenya.