Sakaja yuko tayari kutoa ushahidi dhidi ya maneja wa zamani wa Wendy Waeni

Maneja wa  wa msichana mwanasarakasi mwenye umri wa miaka 14  Wendy Waeni  huenda akajipata katika mgogoro wa kisheria na  baada ya maseneta Johnson Sakaja na  Mutula Kilonzo Junior  kujitolea kumsaidia  mtoto huyo kuthibitisha madai yake dhidi ya maneja huyo  Joe Mwangi .

Kupitia  mazungumzo ya Twitter Viongozi  hao wawili wamesema madai dhidi ya Mwangi yana  vitendo vya uhalifu  na  pia yameibuka wakati viongozi wengine walipotoa ushahidi kwamba huenda Mwangi alikuwa akimtumia vibaya mtoto huyo kwa kuzifuja pesa zake .

Waeni amekuwa akifanya maigizo  ndani na nje ya nchi  na kutangamana na watu mashuhuri . Maisha yake hata hivyo hayajaboreka   kwani yungali anaishi katika mtaa wa Huruma hapa jijini pamoja na mamake.