Salaale! Tazama picha za sherehe ya Akothee iliyogharimu 1.8M

Je ulijua inasemekana kuwa mwanamziki Akothee ndiye mwanamziki tajiri zaidi nchini?

Mwanamziki stadi sana Akothee, alikuwa na sherehe ya kukata na shoka kwenye hoteli ya kifahari ya Kilili Baharini. Sherehe hii ilipangwa ili iwe njia ya kuchanga hela za kuwasaidia wasiojiweza katika kaunti ya Turkana.

Amini usiamini, jamaa tajiri sana kutoka nchi ya Italy, Bwana Massimo, aligharamia sherehe hiyo ya Akothee na kulipa shilingi milioni 1.8 kugharamia sherehe hiyo, iliyofanyika kwa muda wa masaa mawili.

Zaidi ya hayo, Bwana Massimo alikuwa anasherehekea miaka sitini (60) tangu kuzaliwa kwake. Waliohudhuria sherehe hiyo ni mabwenyenye wa kotoka nchi ya Italy.

Mwanamziki mufti wa nyimbo za kitamaduni, bwana Tony Nyadundo, alikuwepo pia, na kuimba nyimbo zake chache za Ohangla kisha akampa nafasi bwana Massimo kuwalisha jamaa na marafiki zake keki ya kuzaliwa kwake. Aisee, sherehe si sherehe bila keki.