Salala! "Ninavumilia kwa sababu alinilipia mahari na akanioa kwa harusi"

Mama mwenye machungu, asimulia mkasa wake.

Shabiki wa Radio Jambo alipiga simu kusimulia machungu yake katika ndoa.

" Nakwambia nimelipiwa mahari mimi.Nimeolewa miaka, sasa ni miaka,huu ni mwaka wa saba.Lakini sasa Annita aki bwana yangu ananisumbua yaani mpaka sasa nashindwa kutoka juu ya iyo mahari nimelipiwa aki nashindwa sasa nikienda watu watasema nini ,watu wa kwetu watasema aje.Alikuwa amenilipia mahari ya 280k na alafu sasa unajua akanioa na harusi.Sasa tumekaka sasa juzi akaanza kupiga umalaya sasa nashindwa.Navumilia juu ya ile hali yaani vile mambo iko inabidi nivumilie.

Mama huyu anaeleza kuwa hawezi toka kwenye boma hilo kwa sababu ya mahari, ndoa na pia anaeleza kuwa watoto wanapenda baba yao sana na kwamba akitoka watoto wataumia.

Siku moja akamwomba bwanake ruhusa ya kwenda kutembea lakini alipofika katika kituo cha gari akajiskia hataki kwenda tena. Akawaacha watoto wake nyumbani kwa rafiki yake. Aliporud ikwake, akampata bwanake na mwanamke mwingine kitandani akavunjika moyo.

Wakaagana na bwanake kwamba wataishi pamoja lakini hawatakusika kimapenzi tena.

" yes ninavumilia lakini sasa mimi na yeye tu tutakuwa sasa lakini mimi mambo ya mapenzi niliweka X.Kila mtu analala bedroom yake, mimi nalala kwa watoto yeye analala hukopekee yake.Akitaka kwenda kulala huko nje mi simuulizi,nilimwambia ukitaka kwenda nenda.Ni miezi sita tangu hicho kitendo kifanyike.Mimi sitoki na hawezi nigusa juu tuliongea na nkamwambia mi ata ukileta mwanamke kwa hii nyumba kitu ntafanya sitoki lakini ukileta mwanamke sitawai kuuliza na wewe usiwai nigusa.

Ni huzuni kwa sababu alipompigia mamake alielezwa kwamba akae huko kwa sababu alishanunuliwa na mamake hakutaka deni. Akaongeza akasema anataka tu bwana huyo awalee watoto.