Sam Nyamweya:Uchaguzi wa FKF ufanywe kupitia ‘Zoom’

Aliyekuwa rais wa shirikisho la soka nchini Sam Nyamweya amesema  amesema uongozi wa sasa wa  soka nchini ndio unaofaa kulaumiwa kwa hatua ya kudorora kwa soka nchini .

Katika mahojiano na radio Jambo  Nyamweya anayelenga  kuwania tena kiti cha urais wa FKF amesema  kiasi kikubwa cha fedha zilizopewa FKF zimetumiwa vibaya  na hapajakuwa na uajibikaji kwa upande wa shirikisho la FKF linaloongozwa sasa na Nicke Mwendwa .akitetea uongozi wake wa miaka mitano alipokuwa afisini ,amesema  hakuwa akipewa ufadhili na aserikali pamoja na shirikisho la fifa kama linavyopewa fedha nyingi shirikisho la sasa .

Amemlamu mrithi wake Mwendwa kwa kumfuta kazi aliyekuwa kocha wa timu ya taifa Harambee stars Bobby Williamson wakati alipochukua usukani  . Nyamweya amesema mamilioni  ambayo serikali  inafaa kumlipa   kocha wa zamani  wa stars Adel Amrouche hazingetolewa  endapo Mwendwa  angefuata ushauri wake .

Amesema  iwapo atachaguliwa kurejea afisini  ataweka mazingira bora kwa wafadhili kurejea katika soka nchini .Nyamweya ameahidi kuwahusisha wadau wote  wa soka kuboresha  mchezo  sio tu kwa  soka ya  wavulana bali pia soka ya akina dada .

Alipoulizwa kuhusu  utendakazi wake alipokuwa uongozini  alijipa asilimia 80  na kusema kwamba anahitaji  nafasi nyingine kujizalia asilimia 20 iliyosalia ili kuboresha  soka ya nchi .