'Samahani kwa kutukana jenerali Badi,'Sonko aomba msamaha baada ya onyo la Uhuru

LVrk9kpTURBXy81MTc4YjkzNTA4NGM3ZDg2MjE5YTk3ZmU2ZDJjMDllMS5qcGeRkwXNAxTNAbyBoTAB
LVrk9kpTURBXy81MTc4YjkzNTA4NGM3ZDg2MjE5YTk3ZmU2ZDJjMDllMS5qcGeRkwXNAxTNAbyBoTAB
Vuta ni kuvute imekuwa ikishuhudiwa mara kwa mara kati ya gavana wa kaunti ya Nairobi na jenerali wa  Nairobi Metropolitan Services (NMS) Mohammed Badi.

Sonko aliomba msamaha na kusema maneno haya saa chache baada ya kukutana na rais Uhuru Kenyatta katika mtaa wa KICC.

"Nataka kusema kuwa nimemsikia rais Uhuru Kenyatta na nimekubali kuwa mahitaji na kaunti ya Nairobi ndio muhimu kuliko wanasiasa

Nataka kuomba msamaha kwa ndugu yangu Badi kwa mambo mabaya ambayo nimesema kumuhusu na naahidi tutafanya kazi pamoja ili tuweze kuleta maendelea kwa wakazi wa Nairobi." Alisema Sonko.

Badi alisema kuwa hakuwa na kinyongo dhidi ya gavana Sonko na kwamba alikuwa afanye kazi naye ili kuwasaidia na kuleta maendeleo kwa ajili ya wakazi wa Nairobi na kaunti hiyo.

"Nataka kumshukuru Gavana kwa maana kwa maana tumefutilia mballi ugomvi wetu na baina ya NMS na timu ya gavana, tutafanya kazi na kuhakikisha kuwa wakazi wa Nairobi wamepata mahitaji yao na maendeleo." Badi Aliongea.

Katika hotuba ya Uhuru alimuonya gavana na wanasiasa ambao wanaleta siasa katika sekta hiyo, pia lipongeza timu ya Badi kwa maendeleo ambayo wanazidi kutenda hasa katika maeneo duni jijini Nairobi.

"Nataka kupongeza timu ya NMS kwa maana kwa miezi hiyo mbili wamechimba visima zaidi ya 200 katika maeneo duni hapa Nairobi

Sonko uwache masiasa mingi, Jenerali Badi hataki kiti ya gavana, hataki kiti hata ya MCA hapa Nairobi. Huyu ni jenerali wangu na akimaliza kazi ya Nairobi atarudi katika kambi ya jeshi 

Mfanye kazi pamoja ili wakazi wanufaike. Mimi sina haja na siasa na wale wanataka kufanya siasa lazima wakae kando," aliongeza Rais.