Sarafu mpya: Kwaheri noti mzee za 1,000, CBK yaeleza idadi iliyokusanya

_109025227_gettyimages-1147728297
_109025227_gettyimages-1147728297
Huku zoezi la kubadilisha noti mzee za 1, 000 likifungwa leo Jumatatu, Benki Kuu ya Kenya ina kibarua kigumu kwani asilimia 70 % ya noti hizo bado haijarudishwa.

Inakadiriwa kuwa noti milioni 152.7 kati ya noti milioni 217.6 za noti ya shilingi elfu moja ya zamani bado zipo katika mzunguko wa fedha.

Nia na azma ya serikali kufutilia mbali matumizi ya noti mzee za 1,000 ni kutatua swala la uhalifu na wizi wa fedha.

Aidha, mpango unakwenda sawa na katiba ya kuipa sarafu sura mpya.

Utafiti unabaini kuwa Kenya imekuwa ikipoteza dola Milioni 400 kila mwaka.

Soma hadithi nyingine:

Pesa hizi zimekuwa zikipotea kupitia biashara haramu.

Dkt. Patrick Njoroge ambaye ni gavana wa Benki kuu ya Kenya ametoa taarifa hizi za kutopata idadi yote ya elfu hizi katika mahojiano.

Kesho Jumanne ndiyo siku ya mwisho ya kutumia noti mzee za 1,000.

Mpango huu ulianza mwezi wa Juni na wakenya wakapewa kipindi cha miezi minne kubadilisha noti hizo.

Uhalifu wa kiuchumi, ulaji rushwa ni kati ya sababu za kubadilisha noti hizi.

Soma hadithi nyingine:

Gavana wa Benki Kuu ya Kenya Patrick Njoroge hapo awali aliwaomba wakenya wawakumbushe wakongwe katika jamii wawajibike katika zoezi hilo.

“Wamama ,nyanya wetu wanapenda kuwekeza sana. Kuna uwezekano wana noti hizi mzee nyumbani.” Njoroge alichapisha ujumbe kwa Twitter.

Noti hizi zikifikishwa katika tawi za Benki Kuu ya Kenya, zitasafirishwa katika lori hadi kwenye makao makuu.

Noti hizi mzee zitapokelewa, kukaguliwa na baadae kuwekwa katika chumba kisicho na oksijeni chini ya ulinzi mkali.

Soma hadithi nyingine:

Maafisa wakubwa watapanga siku na ambayo watakusanya noti zote.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, noti hizi mzee zinakatwakatwa katika vipande vidogo na baadaye kuchomwa hadi ziwe jivu katika eneo la Kariobangi jijini Nairobi.