Sarah Wairimu aomba kurudi Kitisuru, alalamikia uhaba wa mavazi

Sarah
Sarah
Sarah Wairimu ameiomba mahakama kutoa amri ya kupewa gari pamoja na mali nyingine anayomiliki katika jumba la kifahari lenye thamani ya shilingi milioni 400,Kitisuru.

Akirai mahakama, Sarah ambaye alikuwa mkewe Tob Cohen, amesema kwamba hana mavazi na amekuwa akitegemea msaada kutoka kwa marafiki na jamaa yake.

Jumanne, Wairimu alilamikia gharama ya usafiri kwa kukosa gari lake la kibifasi.

Wakili wake Philip Murgor alisema kwamba korti inafaa kuruhusu apewe mali yake.

Akijibu wito huo, mwendesha mashtaka Catherine Mwaniki alisema kwamba hilo ni eneo la tukio la uhalifu na Wairimu hataruhusiwa kuingia jumba hilo.

Alisema kwamba gari hilo ni la ushahidi kwa kuwa lilitumiwa na marehemu.

Aidha mwendesha mashtaka alisema anataka orodha ya mali yote yanayomilikiwa na Wairimu katika jumba hilo ili kubaini kile watakachotumia kama ushahidi.

Jaji Stella Mutuku alimwagiza Murgor kutoa orodha ya mali yote yanayohitajiwa na mteja wake.

Kesi hiyo itaskizwa tena Jumanne ijayo, wakati ambapo korti itafanya uamuzi kuhusu ombi hilo.