Saratani! Mama ajitoa uhai baada kungundua anaugua saratani

Mwanamke mwenye umri wa makano aliyekuwa ameigunduliwa kuungua saratani alijitia kitanzi katika mtaa wa Kasarani, mjini Naivasha.

Wakaazi walioshtuliwa na kisa hicho walimpata mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 38 kwa jina Purity Muthoni alining’inia kwenye kamba katika nyumba ya dadake. Jirani alisema marehemu alikuwa ameeleza rafiki zake kwamba hakutaka kupitia machungu na mateso wanayopitia wagonjwa wa saratani.

Hisia kali zilitawala huku jamaa zake na marafiki wakipokea habari kuhusu kifo chake mwezi mmoja baada ya kuambiwa kwamba alikuwa anaugua saratani. Mama huyo mwenye watoto wawili alikuwa akipokea matibabu katika hospitali kadhaa kabla ya kugunduliwa kwamba alikuwa anaugua saratani.

Habari zingine:

Jirani yake, Anne Nyambura, alisema kwamba Muthoni aliyekuwa akiishi eneo la Olkalau alipata uvimbe kwenye titi lake.

“Alianza kupokea matibabu katika hospitali kadhaa huku uchunguzi wa awali ukikosa kupata tatizo lenyewe hadi pale alipoenda katika hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta mjini Nairobi,” alisema.

Anasema marehemu alikuwa akiishi na dadake anayefanya kazi katika shamba la maua.

OCPD wa Naivasha Samuel Waweru alisema mwili wake ulichukuliwa na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Naivasha.

“ Muthoni akuwa msongo wa mawazo alipopata habari kwamba anaungua saratani hali ambayo huenda ilichangia uamuzi wa kujitoa uhai,” dadake alisema.

Habari zingine:.

Mwishoni mwa wiki jana wakenya waliwapa mkono wa buriani gavana wa Bomet Joyce Laboso na mbunge wa Kibra Ken Okoth waliokuwa wamefariki kutokana na maradhi ya saratani, miezi michache tu baada ya aliyekuwa afisa mkuu mtendaji wa Safaricom Bob Collymore kufariki kutokana na ugonjwa huo.