Sasa unataka kulia?Murkomen wajibizana na Kang'ata

lm3k9kpTURBXy9iMDA4NzhkMjBkNjA5NTlhMDk4ZTk0MmE5MjcwMzMwMS5qcGeRkwXNAxTNAbyBoTAB
lm3k9kpTURBXy9iMDA4NzhkMjBkNjA5NTlhMDk4ZTk0MmE5MjcwMzMwMS5qcGeRkwXNAxTNAbyBoTAB
Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen na kiranja wa wengi katika seneti Irungu Kang'ata Jumanne alizua cheche za maneno kwenye mitandao ya kijamii ya instagram mbele ya kikao cha seneti kuhusu fomula ya ugavi wa pesa.

Inadaiwa kuwa timu ya Murkomen inaunga mkono ugavi wa pesa hasa wale wananufaika kutokana naugavi wapesa katika kaunti.

Kanga'ata alimkejeli Murkomen huku akisema kuwa kaunti kama Nyeri na Mutang'a watapoteza fedha zao ilhali anaunga ugavi wa pesa mkono.

"Linturi na Murkomen ugavi wa pesa utaadhibu kaunti kama Nyeri kwanini? tumekukosea wapi?" Aliandika Kang'ata.

Murkomen naye alikuwa na haya ya kusema,

"Wacha kupagawa na mimi kwa sasa huko kwenye uongozi, heshimu msimamo wangu kama mtu wa nyuma na uongoze."

Kang'ata naye alisema kuwa Murkomen amepinga pendekezo hilo ambapo kaunti 39 zitanufaika na ugavi wa pesa, huku kaunti 8 zikipoteza kutokana na ugavi huo.

"Sasa unataka kulia." Murkomen alimuuliza.

Mjadala wa ugavi wa pesa unaendelea, huku wengi wakingoja kwa hamu nini kitakachotokea.