1.Massawe Japanni
Massawe ndiye mtangazaji wa Kiswahili naayefahamika zaidi kwa kipindi chake ‘Bustani ya Massawe na hasa vitengo vya ‘Ilikuaje’ na ‘Dead Beat’ . Amewavutia wasikilizaji wake kwa sauti yenye mkwaruzo mzuri na pia kicheko che bezo ambacho kinatupa tabasamu . Massawe ni mwanaharakti wa mtoto wa kike na aghalabu msimami yake huwa ya kuwatetea wanawake katika kila hali . Iwapo Radio Jambo ingekuwa ‘Kingdom’ Massawe angekuwa malkia wake .
- 2.Carol Radull
Huyu ndiye Malkia wa soka nchini . Kataa kubali ,hapajatokea mwanadada katika utangazjai nchini ambaye ana ufahamu wa masuala ya soka kama CR. Ucheshi wake wakati wa kipindi cha The Score katika Vituo vya Classic 105 na Kiss FM kila jumamosi ni baadhi ya vinavyowavutia sana mashabiki wa soka nchini . Carol pia amekuwa nguzo muhimu sana miongoni mwa watangazaji na wadau wa spoti nchini waliozua msisimko mpya miongoni mwa mashabiki wa soka nchini kwenda viwanjani kuvishabikia vilabu vya humu nchini . Kando na ufahamu wake kuhusu soka ya ulaya ,CR pia hajakimya kuwakosoa wadau wa soka na waunda sera kwa kufelisha mchezo wa soka na fani nyingine za spoti nchini . Ujasiri wake kusema jinsi mambo yalivyo umemweka katika ligi nyingine ya uanahabari/uanaharakati.
3.Kamene Goro
Mvuto wake hakuna asiyeujua .Mengi yamesemwa kumhusu lakini ukakamavu wake umeshuhudiwa akisema kila kilicho fikrani mwake bila kujali matokeo . Mtangazaji huyo mwenye uzito wa alivyopewa hajachelea kuvuruga mitandao kwa picha zake zake ambazo aghalabu huwaacha wanaume wengi wakidondokwa.Anapiga kipindi cha asubuhi ‘Morning Kiss’ pamoja na dume jingine lenye uzushi Andrew Kibe.
- Terry Muikamba
Mashabiki wake wa Kituo cha Classic wanamfahamu kama Miss Sunshine.Mtoto wa kike ana sauti nzuri na upole wa kuvutia lakini kama hujawahi kumuona anavyotembea kwa msukumo wake wa kimahaba basi hujafika . Hutangaza pamoja na Toto la Kiume ,Mike Mondo, ambaye wanadada hawatosheki na sauti yake .
- Linda Nyangweso
Sauti yake nzuri na lahaja ya kipekee ya lugha hii ya wenyewe imewavutia wengi sana . Ni Mwanadada mtulivu lakini mcheshi pia .Ni mtu siyeweza kubanwa na anasema kilicho kizuri na ukimkosea pia utakipata .
- Cate Sidede
Cate Sidede ni wa kipekee! Sauti nzuri na ukarimu usikadirika . Mtangazaji huyu ni mseto wa urembo na akili. Amekuwa akipiga show ya mid-morning kuanzia saa nne asubuhi hadi saa tisa mchana katika Kiss Fm lakini sasa ameanza maangamizi katika kituo cha Smooth Fm .
7.Njoki Wa Mburu
Huwezi kuikosa tabasamu ya Njoki wa Mburu hata kupitia sauti yake . Njoki ni mtangazaji wa kituo cha lugha ya kikuyu cha Gukena na kwa sasa anapiga kipindi cha asubuhi pamoja na Kajim. Huenda usiweze kusikia lugha hiyo akitangaza lakini ukiisikia sauti na ucheshi wake Njoki,utataka kumpa muda wako .Ni mwanadada mkarimu sana na pia nguzo muhimu sana kwa wasikilizaji wake kuhusu masuala ya kidini/Kiroho. Jumbe zake katika mitandao ya kijamii huwa za kuwapa wafuasi wake matumaini ya kuamini na pia himizo la kutenda mazuri .Njoki wa Mburu ni dhahabu kwa utangazaji wa lugha ya Kikuyu .