Sehemu ya barabara kuu ya Nairobi - Mombasa kufungwa kwa siku nane

Traffic Nyayo Stadium-compressed
Traffic Nyayo Stadium-compressed
Shughuli za usafiri katika barabara kuu ya Nairobi-Mombasa zitaathiriwa kwa kipindi cha siku nane zijazo baada ya mamlaka ya barabara nchini Kenha kufunga sehemu ya barabara hiyo.

Kenha inatarajia kujenga daraja la abiria kuvuka barabara katika mji wa Mlolongo.

Kulingana na mamlaka hiyo, shughuli ya ujenzi inafaa kuanza Novemba 12 na kuendelea hadi tarehe 20 Novemba katika eneo la A8 kwenye barabara kuu ya Mombasa- Nairobi.

Watumizi wa barabara hiyo kuelekea Nairobi wameshauriwa kutumia njia mbadala kulingana na ishara za barabarani zilizobandikwa eneo hilo

Aidha, mamlaka ya barabara za mijini imefungua eneo la barabara kuu ya Southern bypass eneo la Lang'ata ambalo lilikuwa limefungwa awali.

https://twitter.com/KeNHAKenya/status/1194140311888580608?s=20

Barabara hiyo ilifungwa Novemba 9 ili kuruhusu ujenzi wa barabara nyingine ya kuunganisha Lang'ata - Ngong.

Ujenzi wa daraja katika barabara kuu ya Mombasa- Nairobi litarajiwa kupunguza ajali  na kurahisisha usafiri wa watembea miguu.