Sema Mateso! Wakimani aeleza kuhusu mawazo kupindukia, pombe na kuachwa na mpezi wake

Msongo wa mawazo upo na ni tatizo kubwa kwa watu wengi. Mchekeshaji wa zamani  katika kipindi cha Churchill Show Paul Wakimani Ogutu  kwa mara ya kwanza amethibitisha  kwamba amekuwa akipambana na  tatizo la msongo wa mawazo.

Wakimani,  ambaye alikuwa akiendesha gari lake  ambalo lilihusika katika ajali akiwa pamoja na  Emmanuel Makori aka Ayeiya  ambaye aliaga dunia katika ajali hiyo  ameshtakiwa na familia ya  Ayeiya. Familia hiyo inataka awalipe shilingi milioni 21.

Wakimani amesema  baada ya  ajali hiyo alipatwa na msongo wa mawazo na kuanza kunywa pombe. Anasema wenzake katika kipindi cha Churchill show hakuelewa alikuwa akipitia nini wakati huo. Anasema hakuwa na mtu wa  kumtegemea na kaanza kuwa mkali na mwenye ghasia.

‘ Nilipatwa na msongo wa mawazo, mpenzi wangu akaniacha  baada ya kuwa naye kwa miaka mitano. Kuna siku nilikuwa naamka  NA NAANGILIA NAONA TYRES ZA GARI KUMBE NIKO KANDO KANDO YA BARABARA NAANGALIA HIVI NAONA HII NI JAM WATU WANAENDA JOB. NAKUMBUKA NILIBLEKI THE PREVIOUS NIGHT AFTER DRINKING,’  amesema

Aliongeza

kuna siku nilikuwa naamka najipata  NAPIGWA MAKOFI NA MAKARAU NA WATU WAMESIMAMA WANAANGALIA [THERE’S ONE DAY NILIAMSHWA NA MAKOFI KUANGALIA NI POLISI COZ I HAD FOUGHT PEOPLE WHERE I WAS DRINKING THE PREVIOUS NIGHT AND WAS TOLD I HAD FIVE CASES OF ASSAULT.

Amesema hakuna aliyekuwa tayari kumsaidia hata rafiki zake na wenzake hawakujitokeza kumsaidia.

Amewarai mashabiki wake kumsaidia

SPIRITUALLY MUNIOMBEE SANA. I’M STILL ON MY WAY TO RECOVERY.