Sema na Raey: Mimi nikipea mwanaume pesa au nilipe lodging lazima anirudishie tukiachana

anita raeyy
anita raeyy
Mhenga au mkenya yeyote yule aliyekiri kuwa wanawake ni moto wa kuotea mbali hawakutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

Mtangazaji Annitah Raey aliwapa wananawake fursa murwa ya kusimulia iwapo washawahi wanyang'anya bwana zao zawadi walizowatunuku baada ya kutengana.

Cha kushtua ni kuwa wengi walikiri washawahi wanyang'anya wapenzi wao nguo, viatu na hata kudai fedha ambazo walitumia wakati walikuwa wanachumbiana.

Mwanamke mmoja aliwafurahisha wengi alipokiri kuwa alimvua jamaa viatu alivyomnunulia katikati mwa jiji bila aibu. Isitoshe, alimdaisha jamaa mwingine fedha zote ambazo alitumia kulipia chumba cha malazi na pia chakula kwani yeye ana tabia ya kuandika receipt.

Mimi siwezi nunulia mwanaume nguo na nikose kumnyang'anya. Kwanza tukiwachana namzaba kofi na naenda kwake nasanya kila kitu hata kama ni kwa polisi tutaenda.

Pesa zangu haziwezi enda bure, lazima utoe. Kwa sababu atavaa wasichana wamuambie 'You look nice', thank you kwani wewe ndio ulibuy? Zangu lazima utoe siwezi kuwachia na zangu ukinibuyia lazima uniwachie. Alisimulia.

Nilinyang'anya mwanaume viatu kwa mguu, mwingine nilimpeleka police station tukaandikishana naye unajua mimi huandika receipt na nikapiga hesabu yote, alitoa.

Mimi nikipea mwanaume pesa au twende date mahali au lodging huwa naandika hizo pesa ambazo nimetoa ndio tukiachana namwambia lazima atoe. Aliongeza.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be