Sema Na Raey: Mimi nilioa bouncer, bibi yangu alikuwa ananinyorosha!

Daniel Kalua kutoka Athi River aliwashangaza wengi huku akiwachekesha wengine aliposimulia kwa uwazi kuwa yeye alikuwa mwathiriwa wa vurugu za kinyumbani.

Bwana Daniel alisimulia kuwa alijipata akipigwa na mkewe ambaye alikuwa bouncer kila aliporudi nyumbani akiwa amelewa chakari, kwa mda wa miaka mitano.

Isitoshe ni lazima angelala upande wa ukuta kitandani la sivyo angenyoroshwa.

Soma usimulizi wake.

Mimi ndoa yangu ilivunjika last year nilioa mama nikaoa bouncer. Unajua nilikuwa nakunywa kidogo na nikirudi nyumbani hataki nikunywe.

Sasa tukiongea kidogo tukitofautiana ananiambia kuja hapa, ananinyorosha! Ananinyorosha sana mpaka nikaona huyu atakuja kuniua.

Niliishi naye miaka mitano akinipiga, unajua alikuwa bouncer, sasa ikifika wakati wa kulala jioni alikuwa ananiambia nilale kwa ukuta yeye alale hapa mbele.

Tulikuwa na watoto wawili na wote aliniachia na nikawapeleka kwa mamangu mzazi na hashughulikii watoto.

&feature=youtu.be