#SemaNaRaey: Nafanya Kazi Kwa Ofisi Ya Gavana Na Nimelala Na Wasichana 42!

anita raey
anita raey
Ikiwa siku ya Ijumaa siku ambayo kila mtu hujiachilia baada ya wiki nzima ya kazi na kung'ang'ana na maswala ya kisiasa nchini, mtangazaji Anita Raey wa kipindi maarufu nchini; 'Sema Na Raey' aliamua kuwachangamsha waskilizaji wake.

Katika kipindi chake ambacho hujia kwako kwanzia mida ya saa nne hadi saa tisa, Anita alitaka kujua je waskilizaji wake wana wapenzi wangapi na jinsi wanavyo washughulikia.

Mskilizaji mmoja kwa jina Lilian ndiye aliyeanzisha msururu wa mshangao alipofichua kuwa ana wapenzi kumi na saba na kuwa hana shida yoyote kuhusu hilo.

Kulingana naye, kila mpenzi ana kazi yake. Kuna wa kutunza nywele, kuna wa kulipia kucha, wa kulipa kodi ya nyumba na kadhalika huku akisema licha ya hayo ana mpenzi mmoja tu ambaye yeye hulala naye.

"Wanaume wenye nalala nao ni mmoja lakini hao wanaume wengine nikiwaweka kwa mstari ni kumi na saba. Hao wengine kuna wa kunibeba na gari nikienda mahali, kuna wa nguo, kuch, nywele na kuna wa kutuma fedha kwa simu." Alieleza Lilian mwenye umri wa miaka 28.

"Mmoja tu ndio napenda na mimi humuambia kuwa na mpenda lakini hajui kuhusu hao wengine kumi na sita." Aliongeza.

Isitoshe, kuna mwanaume ambaye naye aliwashangaza mamilioni ya waskilizaji huku akidai kuwa amelala na wasichana arobaini na wawili!

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be